Episode Details

Back to Episodes
Taarifa ya Habari:Raia wa Australia azuiwa kimakosa kwa siku 945

Taarifa ya Habari:Raia wa Australia azuiwa kimakosa kwa siku 945

Published 2 days ago
Description
Wito wa kupunguzwa kwa kodi unaongezeka baada ya kura mpya ya maoni kuonyesha wapiga kura wengi wanataka serikali ifanye mengi zaidi kusaidia wapangaji.

Ripoti ya Mchunguzi wa malalamiko wa Jumuiya ya Madola imebainisha kuwa watu 30 walizuiliwa kimakosa na Idara ya Mambo ya Ndani katika mwaka wa fedha wa 2024–25. Miongoni mwao yumo raia wa Australia aliyeshikiliwa katika kituo cha kizuizi cha uhamiaji kwa siku 945, licha ya kuwaambia mamlaka mara kwa mara kwamba yeye ni raia wa Australia.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kupitia mwakilishi wake, imetoa wito tena Jumanne, Oktoba 13, kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kubadili matamshi yao kuwa vitendo ili kukomesha mgogoro uliopo mashariki mwa nchi hiyo. Kulingana na Kinshasa, wakati wa ahadi umekwisha; sasa ni wakati wa utekelezaji mzuri wa ahadi zilizotolewa na pande mbalimbali na maamuzi ya Baraza la Usalama.

Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.
Listen Now

Love PodBriefly?

If you like Podbriefly.com, please consider donating to support the ongoing development.

Support Us