Episode Details

Back to Episodes
Usipuuze Maonyo ya Mungu Kwa Sababu Tu Hayafanani na Matamanio Yako!

Usipuuze Maonyo ya Mungu Kwa Sababu Tu Hayafanani na Matamanio Yako!

Season 3 Episode 20 Published 2 months, 1 week ago
Description

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 1 Samweli 8:18–19 tunaendelea kuona hatari ya kutamani jambo mpaka tusitake tena kusikia kile Mungu anachosema. Samweli amewaeleza Waisraeli wazi gharama ya kuwa na mfalme lakini pamoja na maonyo hayo wanajibu, “Hapana! Tunataka mfalme juu yetu.” Tatizo halikuwa kwamba Mungu hakuwapa mwongozo. Tatizo ni kwamba tayari walikuwa wameamua jibu walilotaka.

Nasi tunaweza kufanya vivyo hivyo. Tunaweza kuomba, “Bwana uniongoze,” lakini moyoni tayari tumeamua tunakotaka kwenda. Tunaweza kutafuta ushauri mpaka tupate mtu atakayetuambia kile tunachotaka kusikia. Neno la leo linatukumbusha kwamba maonyo ya Mungu pia ni sehemu ya upendo wake. Si kila mlango uliofungwa ni kushindwa na si kila “hapana” ni kukataliwa. Wakati mwingine Mungu anatulinda dhidi ya matokeo ambayo sisi bado hatuyaoni. Swali ni hili: Mungu anaposema jambo tofauti na tunalotaka kusikia, tuko tayari kubadilisha uamuzi wetu au tutasisitiza njia yetu?

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Listen Now

Love PodBriefly?

If you like Podbriefly.com, please consider donating to support the ongoing development.

Support Us