Episode Details

Back to Episodes
Waisraeli Walipotamani Kile Wasichokihitaji!

Waisraeli Walipotamani Kile Wasichokihitaji!

Season 3 Episode 19 Published 2ย months, 1ย week ago
Description

๐ŸŽ™๏ธ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 1 Samweli 8:6โ€“7 tunafika katika hatua muhimu katika historia ya Israeli. Waisraeli wanamtaka mfalme ili wawe โ€œkama mataifa mengine.โ€ Samweli anahuzunika lakini Mungu anamfunulia tatizo kubwa zaidi: โ€œSi wewe waliyekukataa bali wamenikataa mimi nisiwe mfalme wao.โ€ Walikuwa na Mungu akiwaongoza lakini wakaanza kutamani mfumo waliouona kwa wengine. Neno la leo linatufanya tujiulize kama nasi wakati mwingine tunatamani vitu si kwa sababu tunavihitaji au ni mapenzi ya Mungu bali kwa sababu tunaona wengine wanavyo. Tunaweza kutamani kazi, fedha, mahusiano, nafasi au maisha ya mtu mwingine mpaka tukashindwa kuona kile ambacho Mungu tayari ametupa. Si kila tunachotamani ndicho tunachohitaji na si kila kitu kizuri kwa mwingine ni kizuri kwa kusudi la Mungu juu yetu. Je, tunaweza kumwamini Mungu hata pale mapenzi yake yanapotofautiana na yale tunayotamani? Wakati mwingine baraka si Mungu kutupa tunachotaka bali kutuzuia tusipate kile ambacho tunadhani tunahitaji.

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. ๐Ÿ™๐Ÿ“–โœจ

Listen Now

Love PodBriefly?

If you like Podbriefly.com, please consider donating to support the ongoing development.

Support Us