Episode Details

Back to Episodes
Hata Sasa Bwana Ametusaidia!

Hata Sasa Bwana Ametusaidia!

Season 3 Episode 17 Published 2 months, 1 week ago
Description

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 1 Samweli 7:12 tunafika katika wakati wa ushindi baada ya Israeli kumrudia Mungu. Samweli anasimamisha jiwe na kuliita Ebeneza, akisema, “Hata hapa Bwana ametusaidia.” Jiwe hilo lilikuwa ukumbusho kwamba hawakufika pale kwa nguvu zao wenyewe bali kwa msaada wa Mungu. Nasi tunapoitazama safari ya maisha yetu kuna milima tuliyodhani hatutaivuka, milango tuliyodhani haitafunguka na nyakati ambazo hatukujua tutafikaje kesho. Lakini leo tupo hapa. Neno la leo linatufundisha umuhimu wa kukumbuka uaminifu wa Mungu kwa sababu kumbukumbu ya kile Mungu alichotenda jana hutupa imani ya kumwamini kwa yale yaliyo mbele yetu. Je, unapoitazama safari yako unaweza kutambua Ebeneza zako na kusema, “Hata hapa Bwana amenisaidia”? Kama Mungu amekuwa mwaminifu mpaka hapa, tunaweza kumtumainia pia katika hatua inayofuata.

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Listen Now

Love PodBriefly?

If you like Podbriefly.com, please consider donating to support the ongoing development.

Support Us