Episode Details

Back to Episodes
Mungu Bado Anaandika Sura za Hadithi ya Maisha Yako

Mungu Bado Anaandika Sura za Hadithi ya Maisha Yako

Season 3 Episode 8 Published 2Β months, 3Β weeks ago
Description

πŸŽ™οΈ Leo kwenye Neno la Leo

Leo tunaendelea na wimbo wa Hana kupitia 1 Samweli 2:6–8. Hana anaposema kwamba Bwana hushusha na kuinua, hufukarisha na kutajirisha, hazungumzi kuhusu Mungu ambaye amesikia habari zake tu. Anazungumza kuhusu Mungu ambaye amemwona akibadilisha maisha yake mwenyewe. Mwanamke aliyekuwa akilia kila mwaka huko Shilo sasa amekuwa ushuhuda kwamba hali ya leo si lazima iwe mwisho wa hadithi yetu. Kupitia simulizi yake tunajifunza kutohukumu kesho yetu kwa changamoto tunazoziona leo kwa sababu Mungu bado anaweza kuinua, kurejesha na kufungua sura mpya ambayo hatukuiona ikija. Je, kuna eneo la maisha yako ambalo umeshaamua haliwezi kubadilika? Usiweke nukta mahali ambapo Mungu bado anaandika.

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. πŸ™πŸ“–βœ¨

Listen Now

Love PodBriefly?

If you like Podbriefly.com, please consider donating to support the ongoing development.

Support Us