Episode Details

Back to Episodes
Usiishie Kupokea Baraka, Mjue Mtoa Baraka!

Usiishie Kupokea Baraka, Mjue Mtoa Baraka!

Season 3 Episode 6 Published 2Β months, 3Β weeks ago
Description

Leo kwenye Neno la Leo

Leo tunaanza wimbo wa Hana kupitia 1 Samweli 2:1–2. Baada ya kusubiri kwa uvumilivu, kupokea muujiza na kumrudishia Mungu Samweli, Hana anafanya jambo kubwa zaidi: anamwabudu Mungu. Cha kushangaza ni kwamba wimbo wake hauzungumzi sana kuhusu mtoto aliyempata bali kuhusu ukuu, utakatifu na uaminifu wa Mungu. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba lengo la mwisho la baraka si kutufurahisha tu bali kutuongoza katika kumjua Mungu zaidi. Je, tunafurahia zaidi zawadi tulizopewa au tunamkaribia zaidi Yeye aliyetoa zawadi hizo? Kwa sababu baraka zinaweza kupita, lakini Mungu hubaki kuwa Mwamba wa maisha yetu milele.

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. πŸ™πŸ“–βœ¨

Listen Now

Love PodBriefly?

If you like Podbriefly.com, please consider donating to support the ongoing development.

Support Us