Episode Details
Back to EpisodesMaridhiano ya kisiasa nchini Tanzania yatafanikiwa ?
Published 3 months, 3 weeks ago
Description
Nchini Tanzania, maneno maridhiano na Katiba mpya, yameendelea kutawala vinywa vya wanasiasa na wananchi wa taifa hilo baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na vurugu wa Oktoba mwaka 2025. Hivi karibuni, rais Samia Suluhu Hassan alikutana nna viongozi wa vyama vya siasa na kutangaza mpango wa maridhiano na mchakato wa katiba mpya. Je, haya yanawezekana bila ushiriki wa chama cha upinzani CHADEMA, ambacho kiongozi wake Tundu Lissu, amezuiwa jela kwa sababu ya kesi ya uhaini ?